Aug 14, 2011

MAKAMUZI YA EXTRA BONGO LEO ALFAJIRI

Wanenguaji wakikata nyonga.
Mwanadada akiserebuka na mpiga gitaa la besi, Osea Msiagi, baada ya kumkuna kwa jinsi alivyokuwa akilicharaza.
BENDI ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kujinafasi, usiku wa kuamkia leo imefanya makamuzi ndani ya Ukumbi wa Meeda…
Wanenguaji wakikata nyonga.
Mwanadada akiserebuka na mpiga gitaa la besi, Osea Msiagi, baada ya kumkuna kwa jinsi alivyokuwa akilicharaza.
BENDI ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kujinafasi, usiku wa kuamkia leo imefanya makamuzi ndani ya Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza, jijini Dar es Salaam. Yafuatayo ni miongoni mwa matukio yaliyojiri kwenye onesho hilo.
Shabiki (kulia), akimtunza Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ wakati akiimba kibao chake cha zamani maarufu kama ‘Mtaji wa masikini’.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ (katikati) akiwa na wakongwe wenzake aliokuwa akiwika nao bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ enzi hizo Rogert Hega ‘Katapila’ (kushoto) na Banza Stone.
Wanenguaji wa zamani wa Twanga waliotimkia Extra Bongo, wakiwa wamepumzika baada ya kushuka jukwaani, kutoka kushoto ni Mwantum Athuman, Aisha Mbegu ‘Aisha Madinda’ na Fetty Kibororoni.
Kiongozi wa wanenguaji wa Extra Bongo, Said Hassan ‘Super Nyamwela’ (kulia) akiwa ameruka hewani wakati safu yake ikishambulia jukwaa.

No comments: