Jul 7, 2011

MSIMU WA DHAHABU WA SERENGETI FIESTA 2011 NDANI YA SHINYANGA

 


Kichwa mahiri katika miondoko ya Hip hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua jukwaani jana jioni kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.Tamasha la Serengeti Fiesta linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd ikishirikiana na Clouds Media Group, wakati huo huo mdhamini mkubwa wa tamasha hilo ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd kupitia kinywaji chake maridhawa kabisa, Serengeti Primeum Lager. Picha inayofuata: Wakazi wa Shinyanga walivyoamua kujiachia vilivyo kwenye tamasha la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta 2011 ndani ya uwanja wa Kambarage jana jioni.
Aaaah! mbona kwa sana tuu...! kitu cha Golden moment kipo hapa.
Msimu wa dhahabu umewakuna vilivyo wakazi wa Shinyanga.
Mkali mwingine wa hip hop Bongo akitokea jijini Arusha, JCB akiwaangushia madini wakazi wa Shinyanga jana jioni.
Shinyanga nayo aaaahhhh....! haina majotro kabisa.
Mh Temba akicheza na shabiki ambaye aliomba apande nae jukwaani.
Wasanii mahiri wa Bongo Fleva Chege na Temba pichani juu na chini wakiwaimbisha wakazi wa Shinyanga kwa namna ya kipekee kabisa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Kambarage, ilikuwa ni full kushangweka bila Majotro kabisa.

Msanii wa kizazi kipya anaekuja juu kwa sasa, Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani.
Mzee wa Robo saa a.k.a Amin kutoka THT akitumbuiza jukwaani na baadhi ya nyimbo zake ikiwemo ya robo saa, bora nikimbie pamoja singo yake mpya iitwayo Mapenzi yameteka dunia.
Mmoja wa mashabiki nae akionyesha umahiri wake wakucheza mtindo wa kiduku jukwaani.
Utulivu ulikuwepo wa kutosha kwa washabiki na watazamaji kama uonavyo pichani.
Msanii mahiri wa kizazi kipya, Mwasiti akiimba pamoja na shabiki wake jukwaani jana jioni ndani ya Uwanja wa Kambarage wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2011 likiendelea.
Wote mikono juuuuuuuuu!!!.
Wakazi wa Shinyanga walivyomwagika kwenye Uwanja wa Kambarage kushuhudia tamasha la msimu wa dhahabu unaoendelea wa Serengeti Fiesta 2011.

Baadhi ya wasanii wa mkoani Shinyanga wakiwa jukwaani tayari kwa amsha amsha za tamasha la Serengeti Fiesta 2011 ndani ya uwanja wa Kambarage.
Ilikuwa full kushangweka kama kawa wala haina majotro kwa wakazi wa Shinyanga.
Mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM/TV, Wasi Wasi Mwambulambo (katikati) akiwa na fundi mitambo, Dj Haroun wa Prime Time Promotions Ltd ndani ya Uwanja wa Kambarage tayari kwa kulianzisha tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Nyomi ikiwa tayari kwa burudani.
Baadhi ya wateja wakiwa kwenye moja ya banda la Serengeti Premium Lager, wakiangusha moja moja taratiiibu bila majotroo wala nini.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya SBL mkoani Shinyanga wakijipanga mikakati ya mauzo ya vinywaji vya kampuni hiyo kwa wateja wao.
Baadhi ya wakazi wa Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa ndani ya Uwanja wa Kambarage kwa ajili ya kushangweka na msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta 2011.

No comments: