Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan huko Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kushoto) wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya wawakilishi wa wananchi kutoka mikoa mbalimbali za Zanzibar kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar uwanja wa Amaan mjini Unguja leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu wa CCM Yusuph Makamba (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) mjini Zanzibar wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanznibar.
No comments:
Post a Comment