Na Maggid Mjengwa,
Ndugu Zangu,
Ni juzi tu nimepigiwa simu na msomaji wangu (RAIA MWEMA) akiwa kijiji cha Mwambata, Masasi. Amejitambulisha kwa jina la Edward Hassan. Alichotaka kuongea ni juu ya suala la Dowans. Suala hilo linagusa maisha yake.
Nikamdadisi juu ya mchanganyiko wa Edward na Hassan katika jina lake. Akaniambia; kuwa huko maeneo ya kusini ni kawaida sana. Utamkuta mtu anaitwa Dominick Rashid, John Ramadhan na mengineyo. Ni majina yanayotokana na dini za kimapokeo toka kwa Waarabu na Wazungu. Ni kweli, maana, Watanzania sisi tuna majina ya asili ya koo zetu. Majina yasiyotokana na dini za kimapokeo. Mengi ni majina yenye maana fulani.
Ndio, Watanzania tumechanganyika kiasi hata kwenye koo zetu tunatofautiana katika imani za kimapokeo; Ukristo na Uislamu. Ni kawaida kabisa katika ukoo mmoja kuwakuta Waislamu na Wakristo. Kinachowaunganisha wanaukoo hawa ni mila zao za jadi ikiwamo matambiko yao. Na leo hii, katika nchi yetu, kuna familia zenye wanafamilia wa imani tofauti za kimapokeo; Uislamu na Ukristo. Ni kawaida kumkuta mama Mkristo na baba Muislamu au kinyume chake. Ni kawaida pia kuwakuta watoto wa familia moja wenye kufuata imani tofauti.
Swali linakuja; hivi wenye kusambaza mahubiri haya ya chuki za kidini wanafahamu kuwa watachochea hata vita vya kikoo? Maana, koo zetu nazo zina tofauti za kidini, hususan dini hizi tulizozipokea toka kwa Wazungu na Waarabu.
Ndugu zangu,
Kuna kila dalili, kuwa sasa baadhi ya viongozi wa kidini na wanasiasa, kwa maslahi yao, wanafanya juhudi za kutugawa Watanzania kwa misingi ya kidini. Tusikubali kugawanywa na tukafikia kuchinjana. Hii ni nchi yetu, na kuna wanasiasa wanaotaka nchi yetu isitawalike. Nchi kutotawalika ina maana ya nchi kuingia katika hali ya vurugu ( State of Anarchy). Hivi, wenye kuombea hili wanaelewa hilo lina maana gani? Watanzania, Wazalendo wa nchi hii, tuna kila sababu ya kuihami nchi yetu dhidi ya chuki hizi za kidini na kisiasa.
Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa na hata kiongozi wa kidini. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi binafsi na ya kundi dogo badala ya yale ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.
Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.
Na hili ni Neno La Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema, juma hili) Fuatilia mjadala na angalia picha http://www.lost-9fm.blogspot.com/

No comments:
Post a Comment