Wiki hii msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘ Diamond’ yupo hapa kujibu na kutolea ufafanuzi juu ya maswali mliyomuuliza.
Aepuke skendo za mademu
Epuka skendo za mademu mdogo wangu kaza buti katika muziki. Selemani Natuku, Dar, 0718803204
DIAMOND ANAJIBU: Kila kitu kinaenda vizuri kwenye kazi zangu za muziki, sishughuliki na mademu.
Huyu anaomba kampani
Diamond napenda kazi zako mzazi ila naomba kampani yako maana nina kipaji cha kuimba. Kabula, Dar, 0683544405
DIAMOND ANAJIBU:Kama una kipaji, njoo Studio ya Sharobaro turekodi nyimbo.
Eti ana ukurutu
Watu wengi wanajua kuwa alikuwa na uhusiano na Jacqueline Wolper lakini siku moja wakati Jack anahojiwa alimponda eti ana ukurutu na anaishi Tandale, unasemaje kuhusu kashfa hizi? Cassian, 0655202202.
DIAMOND ANAJIBU: Sijawahi kuwa na uhusiano na Jack na sina ukurutu mimi ni rais wa usafi na nyumbani kwetu ni Tandale, na hiyo ishu ndiyo kwanza naisikia kwako inawezekana anatafuta skendo kupitia mimi.
Big up
Nakupa hongera kwa kuiwakilisha vyema nchini yetu katika masuala ya malaria, unajiepusha vipi na mademu mcharuko? Wema Mwaipopo, Dar, 0654857882
DIAMOND ANAJIBU: Mimi nakaa na mama yangu mzazi na muda mwingi nakuwa naye, mimi siyo mtu wa kutoka na situmii kilevi cha aina yoyote.
Anapenda majimama
Ni msanii mzuri tatizo ana skendo ya kujihusisha kimapenzi na majimama. Abdi, Dar, 0719463000
DIAMOND ANAJIBU:Siyo kweli kwa sababu nathamini na ninaheshimu sana maisha yangu.
AnajisIkia sana
Napenda kazi zako Diamond na mimi ni shabiki wako namba moja ila nasikia unajisikia sana we wa Mbagala ishi kimbagala. Msomaji, 0787256556
DIAMOND ANAJIBU: Nashukuru, mimi sijisikii kama nilivyo mnyonge kwenye video zangu ndivyo nilivyo.
Katembea na Wolper na Wema
Eti wanasema umelala na Wema Sepetu je, ni kweli na Jacqueline Wolper ni demu wako? Mika Jay, Dar, 0658545470
DIAMOND ANAJIBU: Hapana siyo kweli.
2010 ulikuwa poa, vipi 2011?
Hongera sana kwa kufunika mwaka 2010 vizuri kwa vibao vyako, tutegemee nini 2011. Elia, Iringa, 0718085308
DIAMOND ANAJIBU: Tegemeeni bonge la ngoma kali ya ‘Moyo wangu’ itakayotoka hivi karibuni na kolabo kali nitakayofanya na msanii maarufu kutoka Nigeria.
Ni mkubwa, anadanganya umri
Diamond uko juu lakini unavyoonekana ulidanganya umri wako kuwa umezaliwa 1989 mbona unaonekana mkubwa? Arch, Dar, 0654215214.
DIAMOND ANAJIBU: Ukibahatika kuonana na mimi utaniona, mimi mdogo mdogo tu vyombo vya habari vinanifanya nionekane mkubwa.
Anatumia kondom?
Diamond unaonekana wewe ni mtu wa mademu sana, je unatumia kinga? Mbaruku, Muheza, 0654288656
DIAMOND ANAJIBU: Mimi siyo mtu wa wanawake sema muziki wangu unapendwa sana na wanawake ndiyo unanifanya nionekane nawapenda.
Aende darasani kwanza
Wewe Diamond ingia darasani kwanza usome kwani muziki na elimu vinakwenda pamoja. Msomaji, 0719318495
DIAMOND ANAJIBU: Usijali nitatekeleza hayo.
Aliwahi kuishi na Wolper Kinondoni
Ana skendo ya kuishi na Jacqueline Wolper maeneo ya Kinondoni. Abdi, Dar, 0719463000
DIAMOND ANAJIBU: Siyo kweli, mimi nilikuwa naishi na mama yangu Tandale ila kwa sasa tumehamia Sinza.
Kahamia kwake Mbezi
Alikuwa anaishi Tandale kwao nampongeza kwa kuhamia kwake Mbezi. Martini, Dar, 0766509439
DIAMOND ANAJIBU: Mbezi sijahamia bado lakini nina nyumba yangu huko kwa sasa naishi Sinza.
Amepima ngoma?
Diamond umepima manake unatisha kwa mademu, punguza! Jeni, Dar, 0719038570
DIAMOND ANAJIBU: Juzi tu nimetoka kupima na nilienda na mama yangu.
Ana mafanikio gani mpaka sasa?
Diamond wewe ni mkali tunakukubali, mafanikio yako mpaka sasa ni yapi? Lizo, Moshi,0769286287
DIAMOND ANAJIBU: Nashukuru sana, mafanikio ni mengi kama kukua kimuziki, kujuana na watu wengi, gari, kiwanja, nyumba na mengineyo.
Kabila lake
Diamond wewe ni kabila gani. Didas Asenga, Arusha, 0756952113
DIAMOND ANAJIBU: Mimi ni Mmanyema wa Kigoma.
Alimtosa mpenzi wake Sara
Ninavyomjua Diamond alishawahi kuwa na uhusiano na Sara kabla hajajulikana alivyotoka kimuziki alimtosa. Sabrina, Dar, 0716771215
DIAMOND ANAJIBU: Sara ndiyo mwanamke niliyemuimba kwenye ‘Kamwambie’ baada ya yeye kunitenda alivyoona nimetoka akarejea na mimi nikamkataa kama alivyonikataa.
Historia yake kwa ufupi
Napenda kujua historia yako kwa ufupi. Jumaa Kiju, Tanga, 0784635425.
DIAMOND ANAJIBU: Nimezaliwa miaka 22 iliyopita jijini Dar es Salaam, muziki nilianza tangu nikiwa shule ya msingi kwa kuimba kwenye matamasha mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kila Jumamosi ‘Talent Show’. Nilipoingia sekondari mama akaniambia niachane na muziki baada ya kuhitimu kidato cha nne 2007 ndiyo nikaingia kwenye muziki mpaka leo.
Sasa abadilike
Diamond ni msanii mzuri na nyimbo zako zinavutia ila jaribu kubadilika kwani staili yako ya uimbaji ni ileile. Rama Gamba, Dodoma, 0717752122
DIAMOND ANAJIBU: Usijali, nimesikia ushauri wako na nitaufanyia kazi.
Nitarejea itatoka lini?
Wewe ni mkali big up sana, vipi kuhusu video ya Nitarejea inatoka lini? Win, Iringa, 0655873108
DIAMOND ANAJIBU: Asante, video ya Nitarejea inatoka leo Jumatatu.
Huyu anamkubali ile mbaya
Kaka nakukubali sana japo wanafiki walizusha sana kwamba unaiba nyimbo lakini wewe hukusita ukazidi kukaza buti, nakupa big up sana. Msomaji, 0712700211
DIAMOND ANAJIBU: Asante sana na ninashukuru kwa kuwaambia watu ukweli.
Asilewe sifa, akaze buti
Asilewe sifa kwa kupewa tuzo kwani hajawa staa, akaze buti awe kama profesa J. Nova. Iringa, 0715174247
DIAMOND ANAJIBU: Nashukuru kwa ushauri wako.
Hamjui baba yake
Eti kweli Diamond baba yake hajulikani kwa sababu alikataliwa tangu yupo tumboni kwa mama yake? Khamis, Zanzibar, 0718109106
DIAMOND ANAJIBU: Kweli.
Elimu yake vipi?
Diamond ana elimu gani, mzaliwa wa wapi, vipi suala la ndoa lipo akilini mwake au ni play boy? Hailat, Dodoma, 0763367406
DIAMOND ANAJIBU: Nina elimu ya kidato cha nne, nimezaliwa jijini Dar es Salaam kuhusu ndoa suala hilo lipo akilini Mungu akinifikisha ninapotaka.
No comments:
Post a Comment