
Katika hali iliyojaa maswali na sintofahamu, Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo hivi karibuni alikutwa akiwa katika kampani na vijana wa kiume wawili ambao walijipodoa ‘kupita maelezo’, Risasi Jumamosi lilikusanya ishu.
Tukio hilo lilijiri Januari 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar ambako kulikuwa na ‘bethdei’ ya kutimiza miaka mitano kwa Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania ‘THT’.

“Jamani, wale jamaa waliokaa na Jokate ni Watanzania kweli? Mh!” Alihoji mwalikwa mmoja aliyekuwa akipita karibu yao.

“Ni Wabongo ndiyo, kwani vipi?” Alihoji Paparazi wetu.
“Noo! Unajua vijana wetu Bongo wengi hawajipambi kiasi kile, wale wamezidisha bwana, doo! Wamejipodoa mpaka basi!” Alisema msanii huyo ambaye kwa sasa ‘ametundika daluga ukutani’.

Ilifika wakati, Paparazi alimvaa Jokate na kumuuliza uhusiano wake na vijana hao ambapo kabla ya kujibu aliachia tabasamu kwanza kisha akasema;
“Huyu ni mdogo wangu, yule ni jamaa yake.”
Kuna wakati Jokate alikuwa mbali na jamaa hao ambapo mwandishi alikwenda kumuuliza ‘ndugu’ wa Jokate kama madai ya mrembo huyo kuwa wao ni ndugu yana ukweli wowote.

Alipomuuliza ukaribu wao unatokana na nini, alijibu: “Basi tu, mtu wangu.”

No comments:
Post a Comment