pombe aina ya konyagi kupita kiasi.
Mashuhuda wa tukio hilo
wameimbia malunde blog kuwa tukio hilo
la kusikitisha limetokea siku ya krismasi
Desemba 25 mwaka huu saa moja jioni.
Wamesema marehemu alikuwa anakunywa pombe na wenzake
katika moja ya Glosary mjini Shinyanga na baadaye mwenzao alizidiwa na
kulazimika kurudishwa nyumbani kwake ili akapumzike na hali ilipozidi kuwa mbaya wakampeleka katika hospitali ya
mkoa lakini akafariki dunia akiwa njiani
Hata hivyo mmoja wa
mashuhuda hao ambaye hakutaka jina lake litajwe
amesema kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa anashindana na wenzake kunywa
pombe maarufu konyagi ama wengine wanapenda kuziita Bapa.
Diwani wa kata ya Ngokolo mjini Shinyanga kulikotokea tukio hilo Sebastian Peter
amesema kifo cha God ni mipango ya mungu kutokana na kwamba marehemu hakuwa
mgeni wa pombe na kwamba inadaiwa kuwa kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa
analalamika kusumbuliwa na vichomi siku hiyo.
Akizumgumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa
wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa alikiri kuupokea mwili wa marehemu muda wa saa moja jioni Desemba 25
mwaka huu,akiwa tayari amefariki dunia na kesho yake Desemba 26 ndugu wa marehemu
walifika hospitalini hapo na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi
hivyo kushindwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini chanzo cha kifo
hicho.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema bado hajapata taarifa kuhusu tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki
wa karibu na marehemu anayejulikana kwa jina la John tayari mwili wa
marehemu God Shaini umesafirishwa kwa ajili
ya mazishi hapo kesho nyumbani kwa mama yake
Mabatini mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment