Mar 5, 2012

KIGOGO WA IKULU UDENDA WAMTOKA KWA MASTAA HAWA

 
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
 
Rachel Haule ‘Recho’.
 
Shilole.
 
Nuru Nasor ‘Nora’.
Imelda Mtema na Shakoor Jongo
NAMBA 0712-027214 ni ya kigogo mmoja anayedai kuwa ni mtumishi wa Ikulu (jina linahifadhiwa kwa sasa), ambaye amekuwa akichafua taasisi hiyo kwa kuwatongoza mastaa wa kike Bongo, Ijumaa Wikienda linaifumua.
Mwanzoni alianza kwa kupiga simu kwa waandishi wetu akiomba namba za mastaa aliokuwa amewaorodhesha kwenye listi yake, lakini akagonga mwamba.
Baadaye alipofanikiwa kupata namba za mastaa hao alipiga tena kwa mbwembwe akidai kwamba pamoja na mwandishi huyo kumnyima namba, amefanikiwa kupata za mastaa kadhaa.
LISTI YA MASTAA NI NDEFU
Alitaja listi ya mastaa ambao amelenga ‘kuwalamba’ kuwa mbali na mwigizaji Nuru Nasor ‘Nora’ ambaye ameshalalamika kuwa kigogo huyo anamvunjia ndoa yake, wapo wengine kama Elizabeth Michael ‘Lulu’, Blandina Chagula ‘Johari’ Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, Halima Madiwa ‘Anti Suzy’, Rachel Haule ‘Recho’, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu na wengine kibao wanaowika kwenye filamu za Kibongo.
NI MTU HATARI KWA MASTAA
Baada ya kupata namba zao, jamaa huyo hatari kwa mastaa amekuwa akiwasiliana nao kwa mpigo huku wengine wakimtolea nje na baadhi kudaiwa ‘kuminya’ kwa sababu zao binafsi.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mastaa tofauti ambapo baadhi walikiri kuijua namba ya jamaa huyo na kuwa huwa inawasumbua sana.
“Namba za watu kama hao huwa ni nyingi lakini kwa upande wangu mara nyingi sipokei namba ambayo siijui,” alisema Aunt Ezekiel.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta jamaa huyo, mbali na kukwepa kwa kuomba atumiwe meseji ambazo hakuzijibu, lilimbana ambapo alikiri kutongoza mastaa mbalimbali, kisha akakata simu.
SIRI NZITO
Gazeti hili limekuwa likimchimba mtu huyo ili kujua kama kweli ni mtumishi wa Ikulu ambapo lilibaini siri nzito nyuma yake.
Mbali na kutuma ujumbe mfupi akijifagilia kuwa ni mtumishi wa taasisi hiyo muhimu, pia aliwachambua mastaa wa kike kwa undani kuonesha kuwa ni mtu mwenye data zinazowahusu.

ONYO
Gazeti hili linaiomba Ikulu kuchunguza na kumbaini kigogo huyo kupitia namba hiyo kwani amekuwa akiichafua taasisi hiyo nyeti. Mastaa nao wanapaswa kujihadhari naye kwani inaonekana dhamira yake ni mbaya.

No comments: