Mar 5, 2012

KAMPUNI Y AMAWASILIANO YA ETISALAT YASHINDA TUZO 3 ZA KIMATAIFA

Etisalat Group Chief Commercial Officer and Zantel's Chairman Essa Al Haddad (right) poses with one of the 3 awards Etisalat won for its innovative products in m-health and mobile money in the GSMA Awards held recently in Barcelona Spain. With him are Etisalat Group CEO Ahmed Abdul Karim Julfar (centre) and Etisalat Group Senior Director Products and Services George Held.
Huduma yake ya Mobile Baby yanyakuwa tuzo 2 wakati huduma yake ya malipo kwa kutumia simu yapewa tuzo ya ubunifu
Kampuni ya mawasiliano inayoongoza Mashariki ya Kati, bara la Afrika na Asia imefanikiwa kuonyesha umahiri wake kwenye sekta ya mawasiliano kwa kunyakuwa tuzo 3 kwenye kongamano la mawasiliano linalofanyika kila mwaka Barcelona, Uhispania. Tuzo mbili ni za huduma yake ya ‘Mobile Baby’ ambayo inatoa huduma za afya kwa njia ya simu na tuzo ya tatu ni kwa ajili ya huduma bunifu ya kufanya malipo ya kiasi chochote kwa njia ya simu wakitumia teknologia mpya ijulikanayo kama Near Field Communications (NFC).
Makamu Rais wa Kibiashara Etisalat na Afisa Mkuu wa Kibiashara wa Zantel Ahmed Mokhles alisema ushindi huu ni ishara ya ahadi zake kwa wateja wake kuwa wabunifu kila mara kupitia huduma na bidhaa zake. “Kampuni ya Etisalat imewekeza sana katika teknologia ikiwa na lengo la kubadilisha sura ya sekta ya mawasiliano na inaheshimika duniani kote kwa ubunifu wa bidhaa na huduma zake. Kila mara inakuja na vitu vipya na pekee vinavyobadilisha maisha ya jamii. Kupitia huduma hizi mbili zilizoshinda tuzo tumefanikiwa kufanya hivyo kuleta huduma karibu na jamii kwa muda unaofaa, kwa njia salama na ufanisi mkubwa.” alielezea Bw. Mokhles.
Huduma ya Mobile Baby ni ushirikiano na kampuni ya Qualcomm, D-Tree International pamoja na Great Connection inasaidia kutoa huduma za afya haswa kwa waliyo mbali na huduma za afya na tangu ianzishwe mwaka jana imeonyesha matokeo ya kuridhisha katika kutimiza lengo la millennia la 5 ambalo ni lupunguza vifo vya kina mama na watoto kwa asilimia 75 na kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa wote kufikia mwaka 2015.
Huduma ya Mobile Baby inafanya kazi hivi: Muhudumu wa afya/mkunga kupitia simu yake ya mkononi hujaza eneo alipo, kituo cha afya kilichopo karibu pamoja na taarifa za muuguzi na dereva aliye karibu. Kupitia huduma hii muhudumu wa afya ataweza kuingiza taarifa za maendeleo ya akina mama wajawazito wa eneo lake ambao wamejiandikisha kwenye program hii. Muhudumu pia atawasaidia akina mama kujifunguwa na ataweza kuwasiliana na madaktari kwa njia ya simu kuhakikisha anazingatia kanuni za uzazi salama. Wakati wa dharura ataweza kumsafirisha mama hadi kituo cha afya kilichopo karibu na kulipia usafiri kupitiaa huduma ya pesa kwenye simu Ezy Pesa. Huduma hii ilianzishwa kwanza Tanzania mwaka jana mwezi wa tisa kupitia mtandao wa Zantel na takwimu zinaonesha kwamba kumekuwa na punguzo la asilimia 30 la vifo vya akina mama na watoto.
Mafanikio ya huduma ya Mobile Baby nchini Tanzania, Nigeria, Milki za Kiarabu na Afrika Kusini Etisalat ina mpango wa kuanzisha huduma hii kwenye mashirika yake mwaka huu wa 2012 nchi zifuatazo Afghanistani, Pakistani, Sri Lanka, Ivory Coast, Benin, Togo, Niger na Gabon.

No comments: