Feb 28, 2012

WAKATI NDOA ZIKIWA GUMZO MTAANI WAZAZI WA “BABY MADAHA” WAMTAKA AFUNGE NDOA HARAKA…!!


Posted on 28 February 2012
MSANII mwenye matukio tata ndani ya bongo movie, Baby Madaha, amedai kuwa wazazi wake wanamtaka afunge ndoa lakini kwa upande wake bado hajafikilia kama anaweza kuolewa kwa miaka hii.

DarTalk ilimtafuta msanii huyo ili kujua ishu yake imefikia wapi tangu wazazi wake walipomtaka kufunga ndoa haraka iwezekanavyo, ambapo alisema kuwa hawezi kufuata kila kitu wanachotaka wazazi wake kwani yenye anamaisha yake.

Alisema kuwa kikubwa wanachotaka wazazi wake ni mtoto kwani kaka zake wote tayari wana watoto kitu ambacho kwa uoande wake wanahisi kama hana uwezo wa kuzaa.

“Wazazi wangu wanataka niolewe mapema na lengo lao niwahi kuzaa lakini mi bado sitaki kuanza kulea kwa sasa, na hadi hivi napozungumza wameninunia hawataki kuzungumza na mimi kitu ambacho kinanipa wakati mgumu,” alisema.

No comments: