Mar 18, 2011

SHARO MILIONEA:‘Kamata mwizi meen’ ni swaga tu!

Wiki hii tunaye mkali wa kuchekesha Bongo aliyejipatia umaarufu kutokana na staili yake inayoitwa ‘Kamata mwizi men’ anayeliwakilisha Kundi la Bongo Super Stars Comedy. Mshikaji anafahamika kwa jina la kisanii la Sharo Milionea lakini jina lake halisi ni Hussein Mkiety.

TQ: Kwanza mashabiki wa safu hii wangependa kujua historia yako kwa ufupi.

Sharo:  Ok! Wananiita Sharo Milionea a.k.a Muuza sura, mpaka poda. Nilizaliwa Muheza Tanga mwaka 1987, baadaye nilijiunga na Shule ya Msingi Lusanga kisha nikabukua Sekondari ya Kwabutu zote ziko TA. Nilipomaliza nikajitupa Bongo kumfuata ‘maza angu’.
TQ: Ilikuwaje ukajiunga na sanaa?

Sharo: Muonekano wangu uliwafanya watu wengi wanisukume kuingia kwenye fani hiyo na hatimaye mwaka 2004 nikaamua kujitupia rasmi huku.
TQ: Kufanya sanaa kunaambatana na kupata umaarufu vipi  kuhusu usumbufu wa  totoz.

Sharo: Kimtindo usumbufu upo tena mkubwa, wengi wanajua mkwanja upo so mimi nawapotezea.
TQ:Unataka  kutuambia huna demu wala hujaoa?

Sharo: Sijaoa nasubiri wakati ufike, lakini kimtindo mpenzi ninaye ila kwa sasa siwezi kukutajia jina.
TQ: Unaweza kutuambia ukiwa naye ‘uwanjani’ akikufanyia nini unakuwa hoi?

Sharo: Siwezi kusema lakini kiukweli namkubali kwa kuwa ana vitu adimu ambavyo naamini siwezi kuvipata kwingine.

TQ: Staili unayotumia katika kuigiza umeiga kwa mtu yeyote?
Sharo: Sijaiga kwa mtu, ni ubunifu wangu tu ndiyo maana staili yangu imakubalika sana.

TQ: Kuna wanaodai kuwa umetokea kwenye familia bora, kuna ukweli katika hili?

Sharo:Ni muonekano tu, mimi ni mtoto wa kitaa, maisha yangu siyo uhakika kiivyo.

TQ: Ni kweli kwamba ukiibiwa huwezi kumfukuza mwizi wala kumpigia makelele ili akamatwe?

Sharo: Mimi nakimbia sana, jaribu kuniibia uone, lakini  kimtindo ndo ile kamata mwizi meen! Kamata mwizi babu ni swagga za kutafuta mkwanja.
TQ: Ukiambiwa uwataje masharobaro wengine unaowakubali utamtaja nani na nani?

Sharo: Kuna watu flani wanajua kutupia bling na  mtu mwingine anaiga tu lakini kimtindo Bob Junior, Mr Blue, Mlela Hemed, B12, Mchomvu na Diamond wanajua.

TQ: Nini wito wako kwa wasanii wenzako wa vichekesho Bongo?
Sharo: Kimsingi tuwe wabunifu zaidi, naamini hilo litatusaidia kufika levo za akina Mr Bean na wakali wengine duniani wanaozitengeneza kupitia fani hii.

No comments: