Sexy lady katika miondoko ya Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amedai kuwa yuko tayari kuolewa na staa wa Big Brother Africa ‘All Stars’ 2010, Mwisho Mwampamba, endapo atatimiza vigezo na masharti.
Mrembo huyo aliliambia Ijumaa juzi jijini Dar es Salaam kuwa, kwasasa uhusiano uliopo kati yake na Mwisho ni wa kawaida tu na hawajaingia katika masuala ya ‘ulavidavi’.
Baby Madaha alidai ukaribu wake na Mwisho umewafanya baadhi ya ‘washakunaku’ kuhisi ni wapenzi huku wenyewe wakiwashangaa na kuwachukulia poa.
“Ukweli nampenda sana Mwisho, ni mtu mcheshi, ana tabia ambazo napenda mume wangu awe nazo,” alisema staa huyo wa Songi la Amore.
Wiki kadhaa zilizopita, gazeti hili ndilo lililokuwa la kwanza kuripoti ukaribu kati ya mastaa hao ambapo, Mwisho alikutwa chumbani kwa mrembo huyo jambo lililoibua viulizo kibao.
No comments:
Post a Comment