Jan 6, 2011

AIBU 2011 !

Mwaka 2011 ulipobisha hodi wengi walisherehekea kwa namna mbalimbali lakini kilichotokea Ufukwe wa Coco, Kinondoni, Dar es Salaam ni aibu.

Katika tukio hilo, warembo wanne ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, walifanyiwa vitendo vya ubakaji kwenye maji (baharini), watatu walipopata nafasi walikimbia, mmoja (pichani) akatenda jaribio la kujiua.

The Udaku Master, Ijumaa linamiliki ‘data’ timilifu kuwa kundi kubwa la wanaume liliweka mtego ufukweni hapo na kuendesha vitendo vya aibu bila kushtukiwa.

ILIMUUMA AKATAKA KUJIUA
Habari zinasema kuwa warembo hao wakiwa katika kampani yao ya ‘kutafuna bata’, walijimwaga baharini kuogelea bila kujua kwamba wameingia kwenye anga za wakware.

Data zinamwagwa kuwa warembo hao wakiwa ndani ya maji, kundi hilo la wanaume liliwateka hadi kina kirefu kisha kuwadhalilisha.
“Wale wanaume walikuwa wengi, kwahiyo waliwavua nguo na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji, kwa kweli ilikuwa ni aibu,” mtoa habari wetu alisema.

Aliendelea kusema: “Baadaye warembo watatu walifanikiwa kukimbia lakini huyo mmoja wakabaki naye. Walimfanyia vitendo vibaya kupita kiasi ndiyo maana alipopata nafasi alikimbia na kutaka kujiua akiwa mtupu.

“Alikimbia mpaka barabarani akajitupa agongwe na gari lakini aliokolewa na raia wema ambao walimtafutia nguo wakamsitiri.”

NI TABIA SUGU
Kabla ya tukio hilo, Ijumaa lilikuwa linafanyia kazi madai ya kwamba katika ufukwe wa Coco, kuna kundi la wanaume wenye tabia ya kubaka warembo.

Ilielezwa kuwa kundi hilo la wanaume huwateka wanawake wanaoogelea na kuwapeleka kina kirefu kisha kuwalazimisha kufanya nao mapenzi.
“Ni ngumu kwa mwanamke akiwa kina kirefu kukataa kufanya mapenzi nao kwa sababu ya kuogopa kuzama,” chanzo chetu cha habari kilitonya.

Kiliendelea: “Wakati mwingine mwanamke akigoma humuacha kwa muda atapetape baharini halafu humuokoa na kumpa sharti la kukubali kufanya nao mapenzi.”

SOMO KWA WAZAZI
Shuhuda wa tukio la warembo waliodhalilishwa baharini, Don Sabba alisema: “Wazazi wawe macho na hili, siyo kuruhusu watoto wao hasa wa kike kuja ufukweni bila ulinzi wowote.

“Vijana wengine wana hulka mbaya kupita kiasi na tunaomba serikali iwachukulie hatua hao wabakaji.”

No comments: