Pages

Jun 27, 2011

SERENGETI FIESTA 2011, MWANZA! MWANZA YAFANA


MWANAMUZIKI wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard ‘Shaggy’ akiendelea kuwapagawisha wakazi wa jiji la Mwanza. Na kweli ikuwa ni show ya usisimua na ni historia kwa wakazi wa jiji la Mwanza kwa kupata kitu kitamua katika burudani ni imebaki gumzo kwa kila mtu akiadithia. Shukrani nyingi ziende kwa wadhamini wakuu Serengeti Breweries Ltd, Gapco, Precision Air, Prime Time Promotion na Clouds Fm na wafanyakazi wa Clouds Media Group kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha.


Mwanamziki wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard ‘Shaggy’ akiwasha moto ndani ya Serengeti Fiesta 2011,  CCM Kirumba jijini Mwanza.
‘Tanzania, Are you ready??’ hapa alikuwa akiwauliza wakazi wa Mwanza! Mwanza! Mwanza!
Timu nzima ya Shaggy nayo ilikuwa ikiweka mambo sawa, si unajua mambo yote yalikuwa ni ‘live’ hakuna kukopi.
Timu ya Clouds Fm akijiachia ndani ya CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Shaggy akiumbuiza.
 
Nyomi wa watu iliyojitokeza kushuhudia tamasha ya Serengeti Fiesta 2011.
Hapa mambo yalikuwa yamepamba moto! Shaggy kila pande ya uwanja ni Shaggy!, Shaggy! Shaggy!
 
Mwanadada Sasha ambaye ni mmoja ya timu ya Shaggy akimpa tafu!
Hapa mzuka ulikuwa umempanda Shaggy!
Hivi ndiyo ilivyokuwa ndani ya Serengeti Fiesta 2011, CCM Kirumba jijini Mwanza, Mwanza, Mwanza.

No comments:

Post a Comment