Jul 10, 2013

"NASUBIRI WAKATI MWAFAKA WA KUMUONYESHA KIKWETE YA KWAMBA MIMI NI NANI".....HILI NI TISHIO LA KIHUNI LA RAISI KAGAME KWA RAIS KIKWETE


Nikiwa  katika  upekuzi  wangu, nimeshtushwa sana na kauli za  KIHUNI  za Rais  Paul Kagame  dhidi ya  Rais wetu Kikwete na nchi yetu kwa ujumla....

Rais Kikwete ameepuka malumbano na Kagame kwa  kukaa  kimya , lakini inaelekea Kagame  anadhani ukimya wa Kikwete ni uoga kwake  au labda anatafsiri kuwa anadharauliwa.....

Nadhani  huu  ni  wakati  mwafaka  kwetu  sisi  watanzania  kuungana  na  kumuunga  mkono  rais  wetu  juu  ya  huu  UPUMBAVU  wa  Kagame....

Kagame  ni  lazima  atambue  kwamba  watanzania  tupo  tayari  kuilinda  nchi  yetu  kwa  gharama  yoyote  na  kamwe  hatuwezi  kuwa  VIBARKA  wa  Rwanda...

Ifuatayo  ni  Kauli  ya  Kihuni  aliyoitoa  Rais  Kagame  Kwa  Taifa  letu:
-------------------------------------------------------------

.....“Those people [Tanzanian President Jakaya Kikwete] you just heard siding with Interahamwe and FDLR and urging negotiations… negotiations? 


 Me, I do not even discuss this topic, because I will just wait for you [Tanzanian President Jakaya Kikwete] at the right place and I will hit you! He[Tanzanian President Jakaya Kikwete] did not deserve my answer.


 I did not waste my time answering him…It is well known. There is a line you cannot cross, there is a line, a line that you should never cross. It is impossible…”“


It is in these ominous terms that the Rwandan dictator General Paul Kagame threatened to get even with Tanzanian President Jakaya Kikwete, while addressing Rwandan Youth on June 30, 2013 during a summit called “Youth Konnect”“, sponsored by his wife, Janet Kagame.


Relations between Tanzanian President Jakaya Kikwete and Rwandan leaders have soured in the last weeks. On several occasions Rwandan leaders called the Tanzanian President “a genocide and terrorist sympathizer”, “ignorant”, “arrogant”, and “mediocre leader”. 

The relations have deteriorated following the recommendation by President Jakaya Kikwete of open negotiations between Rwandan, Ugandan and Congolese leaders and their respective armed opposition in order to bring durable peace and security in the African Great Lakes region....
 


source..I will Just Wait For You At the Right Place And I will Hit You, Rwandan General Paul Kagame Threatens Tanzanian Jakaya Kikwete

"VYOMBO VYA HABARI HUWA VINAHONGWA NA WAPINZANI ILI VIWAANDIKE VIZURI".....SPIKA WA BUNGE



Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameibuka na kauli yenye utata mkubwa akivituhumu vyombo vya habari kwamba vinahongwa na wabunge wa kambi ya upinzani ili viandike habari zao vizuri.

Bila kufafanua ni kwa jinsi gani wabunge hao wanatoa hongo hiyo mbali tu ya kusema wanatoa kitu kidogo ili waandikwe vizuri, pia alikana kuwakandamiza wabunge wa kambi hiyo na kuwabeba wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wako upande wa serikali.

Alisema hana upendeleo katika uendeshaji wa vikao vya Bunge kama anavyoshambuliwa na baadhi ya watu na kwamba lawama zinazoelekezwa kwake zinatokana na watu kuangalia upande mmoja.

Spika Makinda alitoa ufafanuzi huo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu vurugu mbalimbali zinazotokea katika vikao vya Bunge mjini Dodoma na hasa juu ya kuporwa au kugeuzwa kwa hoja za upinzani.

Spika Makinda alikuwa ametoka kuzungumza na Spika wa Korea Kusini, Kang Chang Hee.

"Ndiyo najua mnapewa 'kitu kidogo' na hawa wanaoanzisha vurugu bungeni, lakini kusema Spika anapendelea hili siyo kweli hata kidogo,"
aliongeza Spika.

Alisema iwapo angekuwa na kawaida ya kuwakandamiza wabunge wa upinzani kwa kiasi kinachosemwa wengi wa wabunge hao wa upinzani wasingekuwapo bungeni.

“Mimi siwapendelei wabunge wa CCM, ningekuwa hivyo hawa wapinzani wasingekuwapo bungeni,” alisema Makinda muda mfupi baada ya kuzungumza na ujumbe wa Bunge la Korea Kusini uliomtembelea ofisini kwake.

Makinda alisema wakati wa kuendesha vikao vya Bunge haitakiwi kuwa na itikadi za vyama na kwamba kufanya hivyo kunaweza kusababisha vurugu.

Wakati Spika akitoa utetezi huo, wabunge wa upinzani kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtupia lawama za wazi hususani wanapokuwa katika vikao vya Bunge kwamba anawapendelea wabunge wa CCM.

Miongoni mwa mambo ambayo Spika Makinda amekuwa akilaumiwa ni pamoja na kukalia zaidi ya taarifa 10 za ushahidi juu ya kauli za wabunge wa upinzani zilizowasilishwa kwake na yeye kuzikalia kwa muda wote bila kusema lolote.

Miongoni mwa ushahidi huo, umo wa mawaziri kusema uongo bungeni.

Pia Spika amekuwa akilaumiwa jinsi mjadala wa hoja binafsi za wabunge wa upinzani ‘zilivyoporwa’ na serikali, kama ile ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, kuhusu mitalaa ya elimu; ya mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam, na hata ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, kuhusu ardhi ya Meru.

Zote hizi ama ziligeuzwa na kupoteza maana yake hali iliyosababisha mvutano mkali bungeni ukiacha picha ya upendeleo wa dhahiri kwa baadhi wafuatiliaji wa mijadala ya Bunge.

Akizungumzia mchakato wa kupata Katiba mpya, Spika Makinda alisema Bunge la Katiba litakutana Novemba, mwaka huu na  litawajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wajumbe 160 ambao hata hivyo alisema sheria haijasema wanapatikana vipi.

Alisema mwezi ujao serikali inatarajia kupeleka muswada wa sheria ili kufanya marekebisho ya namna ya kupata wajumbe hao 160 ambao siyo wabunge.

Spika alisema katika Bunge hilo, yeye hatakuwa mwenyekiti na kwamba wajumbe wenyewe watachagua kiongozi atakayewaongoza.

Kauli ya Makinda iliwahi kusemwa pia na Naibu wake, Job Ndugai, mara baada ya kuahirisha kikao cha Bunge kwenye mkutano uliopita, kufuatia vurugu zilizotokea baada ya hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Mambo ya Nje, Ezekiah Wenje, kutamka kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kina uhusiano na vyama vinavyounga mkono mashoga.

Wakati vurugu zikiendelea nje ya viwanja vya Bunge kwa wabunge wa CUF na Chadema kuzozana, Ndugai alipita ndipo aliulizwa na waandishi Kulikoni, lakini katika hali ya kushangaza, alivituhumu vyombo vya habari kwamba ndivyo vimesababisha hali hiyo.

“Haya yote mmesababisha ninyi waandishi, mnawadekeza sana wabunge wa upinzani, hata wangefanya nini mnawapamba pamba, lakini mkumbuke siku wakiingia madarakani watafanya haya haya wanayofanya leo,” alisema Ndugai bila kufafanua kauli yake.

Kwenye mazungumzo yake na ujumbe wa Bunge la Korea uliomtembelea ofisini kwake, Spika alisema unalenga kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwamo za uwekezaji na kuendeleza uchumi wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Spika wa Korea, Chang Hee alisema nchi yake imepiga hatua kubwa ya maendeleo ingawa haina chanzo chochote cha kuzalisha nishati ya umeme ikilinganishwa na Tanzania.

Alisema Bunge la Tanzania linafanya vizuri kwa upande wa nafasi za viti maalum ikilinganishwa na Korea Kusini ambayo idadi ya wanawake bungeni ni ndogo.

MCHUNGAJI MTIKILA AITAKA ZANZIBAR IRUDISHE GHARAMA ZOTE ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA TANGANYIKA AMBAZO ZIMESAIDIA KUIIMARISHA ZANZIBAR


 Mchungaji Mtikila  amemwandikia  barua  rais Kikwete  akiitaka Zanzibar  irudishe  gharama  zote  za Tanganyika....
Hii  ni  barua  yake:
---------------------------------------------------------
8 July, 2013

HE. MR JAKAYA KIKWETE
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
STATE HOUSE
DSM

THE RESOURCES OF TANGANYIKA SPENT ON THE UNION AFFAIRS AS FROM 26/4/ 1964 AND HELPED THE ZANZIBARI GOVERNMENT TO DATE



This is to ask you urgently to furnish us with the facts and figures as regards the following:


  1. How much has ever been contributed by each side of the union of Tanganyika and Zanzibar from 26th April 1964 to date, to finance the union services including the ministries of Defense , Home affairs, foreign Affairs, Higher education, etc.

  2. How much has been dished out by our treasury to bail the Zanzaibar Govt out of budgetary constraints, such as payment of the salaries of its government workers or meeting its other emergency requirements.

  3. The cost of Tanganyika's electricity which the state of Zanzibar enjoyed gratis from Tanganyika for all the years.

  4. The amount of finances which our treasury has spent on the Zanzibari parliamentarians in the parliament of Tanganyika (labeled as union parliament), including the expenses on their election, their outfit allowances, their monthly remunerations, their sitting allowances for the bunge sessions, the expenses on their vehicle loans, their medical expenses, their colossal retirement benefits and all other privileges which the Zanzibaris enjoyed from the sweat of the people of Tanganyika in the guise of the "Union".

  5. The amount of money which our treasury has dished out to the political parties and/or Zanzibari politicians, be them under the umbrella of the ruling party or the opposition parties.

Your excellency, the information is urgently required for our extremely urgent public interest moves which are underway, which touch on the inalienable right of the people of Tanganyika to their self determination, which is a basic ingredient of their humanity.

We thank you very much for your anticipated maximum cooperation, which will be very contributory to the consolidation of the independence of the people of Tanganyika and protection of their rightful identity, as much as the people of Zanznibar enjoy these inalienable rights, to the extent of their latest constituonal amendment which amounts to pulling out of the so called "Union", SPARING only the links whoch protect their parasitic advantages which are painful yoke on the neck of our mother Tanganyika, being such a political, economic and social tragedy.

We are by copy of this memorandum asking the accountable ministers and the governor of the central bank which is known to have heavily invested in Zanzibar using Tanganyika's resources, to avail the data as promptly as is required in public intrest.

Rev.Christopher Mtikila

NATIONAL CHAIRMAN (DP)

Copy to:

1.Hon Dr William Mgimwa(Mp), Minister for Finace

2.The Hon.Minister of state in Vice president's office responsible for Union Matters.

3.Hon.Benard Membe (MP) Minister for Foreign Affairs

4.Prof.Benno Ndulu, Governor of the Bank of Tanzania

-via  Wavuti

POLISI YAWAZUIA CHADEMA KUANZISHA KAMBI YA KIJESHI KWA AJILI YA KUWAANDAA VIJANA WAKE



Mnamo tarehe 09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao cha kuwalinda ambacho watakipatia mafunzo ya ukakamavu.



Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.



Kufuatia kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake.

Imetolewa na:-

Advera Senso-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

CHADEMA YAJIPANGA KUIMARISHA KITENGO CHA ULINZI NA USALAMA " RED BRIGADE" ILI KUWAKABILI VIJANA WA CCM WATAKAOLETA FUJO


MUHTASARI
Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.
 RIPOTI  KAMILI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE 06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM.

Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura kuanzia tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na mambo mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini.

Kamati kuu imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

1:0. Hali ya Siasa Nchini.

Kamati kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na kuzingatia mambo yafuatayo:

a) Shambulio la Bomu Arusha.

 Kamati Kuu imesikitishwa na kulaani kwa nguvu zote tukio la Bomu Arusha lililosababisha watu wanne kuuwawa na zaidi ya watu 70 wengine kujeruhiwa vibaya.

 Kamati Kuu imeridhika kwamba shambulio hilo lililenga kuwaua viongozi wakuu wa CHADEMA akiwamo Mwenyekiti wa Taifa Mheshimiwa Freeman A. Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mheshimiwa Godbless J. Lema na viongozi na wanachama wengine wa CHADEMA waliohudhuria Mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika Jiji la Arusha pamoja na kuvuruga Uchaguzi huo na kuinyima CHADEMA ushindi mkubwa;

 Kamati Kuu imeridhika kwamba ushahidi uliopo wa vielelezo na wa mashuhuda wa shambulio unaonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa Jeshi la Polisi katika shambulio hilo;

 Kamati Kuu imefadhaishwa na kauli ya Serikali bungeni iliyolenga kulikosha Jeshi la Polisi kwa kuhusika kwake na shambulio hilo dhidi ya CHADEMA na wananchi wa Jiji la Arusha na kuilaumu CHADEMA wakati CHADEMA ndio mhanga wa shambulio hilo;

 Kamati Kuu imeshangazwa na kitendo cha Serikali kupuuza maafa yaliyowafika wananchi wa Arusha kwa kushindwa kushiriki katika mazishi ya wahanga wa mauaji ya Soweto na kuwashambulia kwa mabomu ya machozi, vipigo na maji ya sumu waombolezaji waliokusanyika kuwaaga marehemu waliouawa kwenye shambulio;

 Kamati Kuu imesikitishwa na Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya juu ya shambulio la Arusha na kushindwa kwake kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza kwa uwazi shambulio hilo. Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba ukimya huu wa Rais Kikwete na kushindwa kwake hata kuwatembelea wafiwa na wahanga wengine wa shambulio hilo ni ushahidi mwingine wa kuhusika kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali katika kupanga na kutekeleza shambulio la Arusha;

 Kamati Kuu imefadhaishwa na kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano kuendelea na vikao vya Bunge kama kawaida; kukataa kutoa mchango wowote kwa wahanga na kushindwa kupeleka ujumbe wa Bunge kuwatembelea na kuwafariji wahanga na waathirika wa shambulio kinyume na utaratibu uliozoeleka wa Bunge kutambua na kushiriki katika majanga na misiba ya aina hii.

Kamati Kuu inautaka uongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uwaeleze Watanzania kama maafa ya shambulio la Arusha yalikuwa na tofauti yoyote na maafa ya shambulio la bomu la Olasiti, au na maafa ya mabomu ya Gongo la Mboto, ajali ya MV Skargit au maafa mengine yaliyosababisha Bunge la Jamhuri kuahirisha shughuli zake, kutoa michango kwa waathirika pamoja na kupeleka ujumbe wa Bunge kuwafariji wafiwa na wahanga wa matukio hayo;
Kutokana na maelezo hayo hapo juu Kamati kuu imeazimia kuwa:

• Iwapo Rais ataendeleza msimamo wa kutokuunda tume huru ya kimahakama, Ushahidi uliopo juu ya tukio la kurushwa Bomu Arusha utawekwa wazi muda utakapofika kwa wananchi wa Tanzania; vyama na mashirika ya kiraia ya haki za binadamu hapa nchini na ya nje ya nchi; ofisi za kibalozi za mataifa rafiki na Tanzania pamoja na jumuiya ya kimataifa ili yaishinikize Serikali kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza shambulio hilo na matukio mengine ya mauaji yenye sura ya kisiasa ambayo yamehusishwa na Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama vya Serikali au vya Chama cha Mapinduzi;


2:0. Hali ya Wananchi wa Mtwara.

Kamati kuu imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa juu ya unyanyasaji, utesaji, ubakaji na uonevu wanaofanyiwa wananchi wa Mtwara hivi sasa na vyombo vya dola huku serikali ikikaa kimya juu ya jambo hili bila kukemea. Kamati kuu imejadili kwa kina namna wananchi wa Mtwara wanavyofanyiwa na vyombo vya dola na kufikia maazimio yafuatayo;

 Vyombo vya dola vitimize wajibu wake wa kulinda amani na mali ya raia na siyo kuwatesa na kuwapiga wananchi kwa kuwasababishia vifo kinyume na Haki za Binadamu.

 Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara na siyo kutumia ubabe, unyanyasaji, uonevu na mateso kama mbinu za kuhalalisha kukubalika kwake kwa wananchi.

 Rais Kikwete alitangazie taifa “hali ya hatari” kwa mkoa wa Mtwara kama anaona kuwa Mtwara ni hatari kwa kiasi hicho cha kulitumia JWTZ kuzunguka mitaani na silaha za kijeshi ili taifa liweze kujua,Aidha kama jeshi la polisi limeshindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria atangaze kulivunja jeshi hilo mara moja.

 Serikali iunde tume huru ya kuchunguza matukio ya mauaji,ubakaji,utesaji na ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyofanywa na vyombo vya dola na waathirika wote waweze kufidiwa kwa mujibu wa sheria.

3:0. Kauli ya Waziri Mkuu.

Kamati Kuu imejadili kwa kina kauli ya Waziri Mkuu Bungeni kwamba ni sahihi kwa Jeshi la Polisi nchini kuwapiga Wananchi wote wanaotumia haki zao za Kikatiba kupinga sera au maamuzi ya Serikali. Kamati Kuu imeazimia kuwa:

 Kauli ya Waziri Mkuu imekiuka Katiba na sheria za nchi yetu zinazokataza Jeshi la Polisi kutumia nguvu dhidi ya raia wasiokuwa na silaha na ambao wanatumia haki zao za kikatiba kufanya maandamano;

 Kamati Kuu inaamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu inatoa Baraka kwa Jeshi la Polisi kuendeleza vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya wananchi ambayo yamelifanya Jeshi la Polisi la Tanzania kutangazwa kuwa moja ya majeshi katili ya polisi katika Afrika Mashariki;

 Kamati Kuu inaungana na wananchi, taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa ambayo yamelaani vikali kauli hiyo ya Waziri Mkuu na inawataka wananchi, taasisi na mashirika hayo kuendelea kumlaani vikali Waziri Mkuu kwa kauli hiyo;

 Kamati Kuu inaamini kwamba Waziri Mkuu amepoteza sifa za kuendelea kuwa Waziri Mkuu na inaungana na wananchi na taasisi ambazo zimedai Waziri Mkuu awajibike au awajibishwe kutokana na kauli yake hiyo. Aidha, Kamati Kuu inawaelekeza Wabunge wote wa CHADEMA washirikiane na Wabunge wengine wote wenye mapenzi mema na nchi hii na ambao wanaamini katika utawala wa sheria waanzishe mchakato wa kumpigia kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu kupitia Bunge;

 Kamati Kuu imewataka Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii ya watanzania kupuuza kauli ya Waziri Mkuu katika utekelezaji wa kazi zao kwa kuwa kauli hiyo ni ya uvunjifu wa Katiba na Sheria na inachochea uvunjifu wa amani.

4:0. Uchaguzi wa Madiwani.

Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu ushiriki wa CHADEMA katika Uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 16/06/2013 katika kata 22.

 Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti na uongozi wa Kanda mbalimbali za CHADEMA kwa maandalizi mazuri katika Uchagzuzi huo uliosababisha CHADEMA kuwapokonya CCM ushindi katika kata 4 ilizokuwa imeshinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kamati Kuu imewapongeza wananchi kwa kuipatia CHADEMA kura asilimia (47.7%) dhidi ya CCM (49%) na (3.3%) za CUF.

 Kamati kuu imesikitishwa na vitendo vya fujo walivyofanyiwa viongozi, wagombea pamoja na Wanachama mbalimbali katika sehemu mbalimbali palipo fanyika Uchaguzi. Kamati Kuu imesikitshwa na kulaani vitendo hivyo vikiwemo vya watu kukatwa mapanga , kuchomwa visu na kubakwa kwa akina Mama na vijana wahuni walioandaliwa na Chama cha Mapinduzi.

 Kamati Kuu imelaani vitendo hivyo vya kinyama vilivyofanywa mbele ya jeshi la polisi na Wakuu wa Wilaya.

 Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.

 Kamati Kuu imejadili maandalizi ya Uchaguzi wa madiwani katika kata nne (4) katika Jiji la Arusha. Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko taarifa juu mipango inayofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na viongozi wengine wa CCM mkoani Arusha katika kuhujumu zoezi la Uchaguzi kwa kuwatisha wapiga kura kwa kutumia polisi na vijana wa Green Guard siku ya uchaguzi.

 Kamati Kuu inamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuchukua hatua stahiki kuzuia harakati za polisi na CCM za kuvuruga Uchaguzi na kutaka kujipatia ushindi kwa njia za hila. Aidha Kamati kuu imelitaka jeshi la polisi kuheshimu maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na Serikali, Tume ya uchaguzi na vyama vya siasa.

 Kamati Kuu imesikitishwa na Tume ya Uchaguzi kushindwa kuwazuia CCM kuendelea na kampeni za Uchaguzi huku wakiwa wamezuia kampeni hizo kwa vyama vingine.

 Kamati Kuu imeendelea kuwapa pole wananchi wa Arusha kwa matukio mabaya wanaofanyiwa na serikali ya CCM mkoani humo, na imewapongeza kwa kusimama kidete katika kulinda haki na ukweli.

 Kamati Kuu imewaomba wananchi wa Arusha wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 14 Julai 2013, na imewataka wabunge wote washiriki katika kusimamia zoezi la upigaji kura na uhesabuji kura siku ya Uchaguzi na wananchi wajitokeze kwa wingi kulinda kura bila hofu.

5:0. Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kamati Kuu imejadili kwa kina sana maudhui yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba;

• Kamati Kuu imetambua kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kukusanya na kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya;

• Hata hivyo, Kamati Kuu imetambua na kuainisha mapendekezo mengine ya msingi ambayo yanastahili kuboreshwa zaidi katika Rasimu hiyo;

• Msimamo na maazimio ya Kamati Kuu juu ya Rasimu ya Katiba Mpya yameainishwa na kuchapishwa katika kijitabu maalumu ambacho kitazinduliwa katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika siku, tarehe na mahali patakapo tangazwa hapo baadaye.


Imetolewa na:

……………………….

Freeman A. Mbowe, (MP)

Mwenyekiti Taifa

Jul 8, 2013

"PREZZO ANAYAJUA MAPENZI.....HATA AKINIUTHI SITAHESABU MAKOSA YAKE"....DIVA WA CLOUDS FM


Muda mfupi uliopita mtangazaji wa ‘Ala za Roho’ ya Clouds FM Diva Loveness Love ambaye sasa anatumia “divathebawse” katika akaunti yake ya Instagram, ameweka picha mpya akiwa na Rapcellency Jackson makini aka Prezzo kutoka Kenya waliyopiga jana (July 7).


Picha hiyo ambayo inawaonesha wawili hao wakiwa “0 distance” ilikuwa na caption inayosomeka hivi,

“Nothing Than Happiness… Prez is such a Nice guy. Hata Akiniudhi Sihesabu makosa yake. May you Live Long Pleaseeee……… Good hearted, My hero, My Mentor… A Person I can count to when I need to be happy… No one is Perfect yes but I love his flaws and All…. Bless you always’ . I Pray you live Long… I Pray for you Always”


Picha nyingine iliwaonesha Prezzo na Diva wakikumbatiana na kusindikizwa na caption “Last Night at escape1… I was nothing than happy. With Prezzo”.




Prezzo alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza jana (July 7) katika show ya Matumaini iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

SABABU TANO ZILIZOWAFANYA CHADEMA WAGOME KUSHIRIKI "KONGAMANO LA AMANI" LINALOANZA KESHO


Ndugu waandishi wa habari,
Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharula, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:

Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).

Kongamano hilo linatajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.

Baadhi washiriki ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na Chadema.



Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.

Ndugu waandishi wa habari,
Chadema kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa kutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:

Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa muwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu anaowataka wao.



Pili, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe.

Katika mazingira haya, Chadema inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.



Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadfau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.

Nne, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhiri na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafasi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.


Ndugu waandishi wa habari;
Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.


 Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung’oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi yamaovu.

Tano, Chadema haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhiri mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.
 


Chadema inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, kutaka kukibeba chama hicho.

Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo.


 Ili amani iweze kupatikana, ni sharti tuwe kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ione inachukuliwa na serikali.

Chadema kiko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. Chadema haifanyakazi na wanafiki wa amani.

Imetolewa na:
Benson Singo Kigaila,
Mkurugenzi wa Oganaizesheni ma Mafunzo,
Dar es Salaam

MASANJA MKANDAMIZAJI AFICHUA UBAGUZI WA BANK YA CRDB KATIKA UTOAJI WA AJIRA


Katika  upekuzi  wangu  , niliamua  kumtembelea  masanja  mkandamizaji  kuona  alichokandamiza  jioni  hii...

Hii  ni  post  yake  facebook  iliyofichua  UBAGUZI  wa  bank  ya  CRDB  katika  utoaji  wa  ajira  kwa  wasomi  wetu  hapa  nchini...

------------------------------------------------------------------------

Internship opportunities with CRDB Bank PLC. These opportunities cover different regions/branches all over the country as indicated below.
•Arusha
•Bagamoyo
•Bukoba
•Dar es Salaam
•Geita
•Ifakara
•Karagwe
•Kigoma
•Kilombero
•Makambako
•Mbeya
•Morogoro
•Njombe
•Shinyanga
•Singida
•Songea
•Tabora

Minimum Requirements
Final year student from UDBS also other UDSM Students will be considered
•GPA of at least 3.5
•The applications should comprise CVs, Provisional results, a cover letter indicating the station/branch of preference among the mentioned above.

Due to limited space only shortlisted candidates will be contacted.

Deadline: 10th July, 2013 at 1500hrs

Submission: online (career@udbs.udsm.ac.tz) or B.324 (office hours)

SWALI: TANZANIA KUNA VYUO VIKUU VINGAPI?
------------------------------------------------------------------------
  

UWOYA AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUMFANANISHA DIAMOND NA MICHAEL JACKSON


Mwigizaji  wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.

Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.
 

Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.
 

“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa gumzo mitandaoni.

“Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi) au kwa sababu Diamond amesha…(tusi) ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,” aliandika shabiki mwingine kwenye Twitter na kupisha wengine kuendelea kumporomoshea Uwoya matusi ya nguoni.

MWANAFUNZI WA CHUO CHA VETA MKOANI DODOMA AJILIPUA KWA PETROL.....KISA NI WIVU WA MAPENZI


MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.