Jul 10, 2013

ZITTO KABWE AWATAKA WANANCHI WAGOME KUILIPA KODI YA SIMU YA SH. 1000.....AMEDAI KUWA KODI HIYO ILIPITISHWA KINYEMELA



Sakata  la  kodi  ya  line  ya  simu  limeendelea  kuwakuna wanasiasa  wetu  ambao  wamekuwa  wakifunguka  kwa  nyakati  mbalimbali  kupitia mitandao  ya  kijamii....

Baada  ya  January  Makamba, Zitto  kabwe  naye  amefunguka  na  kudai  kuwa  kodi  hiyo  ni  batili  na  ilipitishwa  kinyemela  kwa  sababu  ilikuwa  imeshaondolewa....

Huu  ni  ujumbe  wake  aliouweka  katika  account  yake  ya  facebook:
Baada ya  kauli  hiyo,Zitto  Kabwe  aliandamwa  na  maswali  mengi  sana  toka  kwa  wananchi  wakidai  kuwa  "Makamba  alisema  tuwalaumu  ninyi  maana  ninyi  wabunge  ndo  mlibariki  kodi  hii"

Zitto  naye  alishindwa  kulijibu  swali  hilo  na  kuwataka  wananchi  "wachukue  simu  zao, wawapigie  wabunge  wao  wawaulize  ni  kwa  nini  walipitisha  kodi  hii"

 "Anasema  hiyo  kwa  sababu  wabunge  ndio waliopitisha.Wabunge  ndio  wawakilishi  wa  wananchi.Jambo likipita bungeni hao ndio wa kwanza kulaumiwa.Yupo sahihi kabisa.Mpigie mbunge wako simu muulize kwa nini  alikubali au  hakupinga kodi hii"..Hili  ni  jibu  za  Zitto Kabwe

No comments: