MWIGIZAJI wa kike na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Baby Madaha Joseph amemshukia mwigizaji mwenzake wa kike Jack Wolper kwa kudai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari kumsema na baadae kujifanya anamuomba msamaha huku hana dhamira ya kweli.
Akiongea na FC , msanii huyo amesema kuwa Jack Wolper anatumia jina lake ili apande na kuwa Maarufu (nyota ).
“Mimi ni mwanamke mpigaji na ninajua ninachofanya katika maisha yangu...
"Kuna wanawake hawajui misingi ya sanaa.Ni wanawake ambao wamevamia fani na kutuharibia sifa zetu kama wasanii..
"Mimi siwezi kugombana na mtu mwenye fani moja ,tena ya kubebwa . Jack hana cha kufanya akifeli kuigiza labda arudie kazi yake ya kuuza vipodozi...Atafanya nini kingine hapa mjini zaidi ya kujiuza?,”alisema Baby Madaha na kuongeza:
“Jack anataka kukiki kwa kunichafulia jina langu, lakini mimi ni Star mwenye vision na najua nafanya nini katika Industry..
"Mimi ni kiongozi mtarajiwa .Nategemewa niongoze watu , sasa nikianza kugombana na watu itaniharibia ndoto zangu za kisiasa,”
FC
No comments:
Post a Comment