Sep 6, 2012

MAN UNITED YAMTENGEA NEYMAR PAUNDI MILIONI 38.


KLABU ya Manchester United imetenga kitita cha paundi milioni 38 kwa ajili ya kumnyakuwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar. Dau hilo ambalo linavunja rekodi ya klabu hiyo, ilishindwa wakati timu hiyo ilipomtaka mara ya kwanza baada ya nyota huyo mwenye miaka 20 anayecheza katika klabu ya Santos kusema kuwa anataka kubakia katika klabu yake hiyo mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 ambapo nchi yake itakuwa wenyeji. Nia ya meneja wa United Sir Alex Ferguson kutaka kumsajili Neymar kunazua maswali mengi juu ya mustakabali wa mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney kwani kocha huyo ameonekana hawezi kushindwa kujaribu kumsajili Neymar tena katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. United imeamua kuhamishia nguvu zake kwa Neymar baada ya kuzidiwa kete na klabu ya Paris St Germain ya Ufaransa katika mbio za kumsajili Mbrazil mwingine Lucas Moura ambaye ana umri wa miaka 19. Ila bado inaonekana kutakuwa na vita kubwa ya kumgombani mchezaji huyo ambaye amefunga mabao 113 katika michezo 190 aliyochezea klabu ya Santos, kwani klabu za Real Madrid na Barcelona nazo zimeonyesha nia ya kumsajili.

No comments: