 |
Ferguson akipiga stori na Bolt. |
MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson yuko tayari kutimiza ndoto za mwanariadha nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica kwa kumjumuisha katika kikosi chake ambacho kinatarajia kucheza mchezo wa hisani dhidi ya Real Madrid. Bolt mwenye umri wa miaka 25 alinyakuwa medali mbili za dhahabu katika mbio za mita 100 na 200 kwenye michuano ya Olimpiki iliyofanyika Agosti jijini London na baadae kumuomba Ferguson kumfanyia majaribio katika klabu yake. Ferguson alimjibu nyota huyo ambaye ni shabiki wa kutupwa wa klabu hiyo kwa kumualika kama mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Fulham mwishoni mwa mwezi uliopita na kutambulishwa kwa mashabiki pamoja na wachezaji wa timu hiyo. Bolt ambaye aliweka rekodi mpya katika mbio za mita 100 kwa kutumia muda wa sekunde 9.63 katika Uwanja wa Olimpiki uliopo katika mji wa Stratford maombi yake ya kufanya majaribio yanaonekana kufanikiwa.
 |
Bolt akisakata kabumbu. |
Akihojiwa na gazeti la timu hiyo Ferguson amesema kuwa alizungumza na Bolt na kumuuliza kama anaweza kucheza mechi ya hisani na akamjibu kwamba anaweza, hivyo itakuwa ni jambo zuri kumtumia katika mchezo wa hisani dhidi ya Madrid ambao utapigwa Januari mwakani na kumuangalia kama ataweza.
No comments:
Post a Comment