Jul 26, 2012

SERIKALI INAPOTEZA TSH 50,000,000 KWA KILA NYIMBO.

Kwa sababu ya Poor copyrights and Income Managment , naamini Serikali Huenda ikawa inapoteza Fedha Zisizopungua Shillingi za Kitanzania Milioni Hamsini (50,000,000.00) kwa kila Watanzania Millioni Moja (1,000,000) wanatumia Simu au Kuingiza nyimbo kwenye simu au kurekodiwa kwenye CD.
Hii ni kwa hesabu zangu za darasa la nne :-
Nyimbo sasa hivi zinaingizwa kwa 200/= hadi 500/= kwenye CD au SIMU / Per Song.
Hivi kama kungekuwa na utaratibu wa kusimamia hizi kazi za wasanii kwa asilimia ndogo tu, unafikiri vijana wangekimbia mashamba?
Banana, Dully, Diamond, Ally Kiba na wengineo wengi wangekuwa na mashamba makubwa na wala kusingekuwa na shida ya chakula.
Anyway, back to my subject.
Kama Kukiwa na usimamizi mzuri naamini kila msanii anaetoa nyimbo na ikasimamiwa vizuri na Serikali au wasimamizi wengine watakaolindwa na serikali basi kila nyimbo inaweza (Rate Ya Watu 1,000,000 tu) :-
Kumpatia Muuzaji / Anayeweka nyimbo kwenye simu : Tsh 150 - 300 kwa nyimbo.
Kumingizia Kipato Msanii : Tsh 50,000,000 kwa nyimbo x (1,000,000 x Tsh 50).
Kuiingizia Kodi Serikali : Tsh 50,000,000 kwa nyimbo = (1,000,000 x Tsh 50).
Ni Hayo Tu.

TAFAKARI - CHUKUA HATUA.

No comments: