BODI ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organization (MTTO), imelifuta
shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, lililo fanyika New Mwanza
Hotel, juzi, huku taifa likiwa kwenye maombolezo ya siku tatu kutokana
na msiba mkubwa wa ajali ya meli ya Mv Skagit, mjini Zanzibar na
kupoteza uhai wa watu wengi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari jana jijini
Dar es Salaam na kutiwa sahihi na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa
Miss Utalii Tanzania, Abubakari Omary Bakari, ilisema shindano hilo
limefanyika kimakosa na matokeo yake hayawezi kutambuliwa kwa namna
moja ama nyingine.
Alisema uamuzi wa serikali ni wa mwisho, hivyo hawajaunga mkono
kufanyika kwa shindano hilo wakati nchi ina majonzi ya kupoteza ndugu
na jamaa wao.
“Shindano limefanyika bila kuzingatia misingi ya kiubinadamu na
uzalendo kwa Taifa, hivyo Bodi imeamua kulifuta na waandaaji watafuata
tena utaratibu mwingine.
“Miss Utalii ni shindano lenye uzalendo, hivyo inapotokea matatizo
kama haya na agizo la maaombolezo kutoka kwenye serikali nadhani kuna
kila sababu ya kuliafiki,” ilisema taarifa hiyo.
Shindano hilo limeandaliwa na Fania Beauty Salon, chini ya Mkurugenzi
wake Fania Hassan, ambaye sasa ana changamoto nyingine ya kujiweka
sawa katika jamii, ukizingatia kwamba Taifa lilikuwa kwenye maombolezo
ya siku tatu

No comments:
Post a Comment