Apr 4, 2011
KUBWA KALIMENZE AFUNGUKA NA MPIRA WA KIKAPU.........AISIHI SERIKALI IWAPE NAFASI
Mpira wa kikapu ni moja kati ya michezo ambayo imesahaulika nchini Tanzania, vijana wakiwezeshwa katika mchezo huu amini usiamini wanaweza wakafanya vizuri kushinda mpira wa miguu ambao umekuwa ukipewa kipaumbele lakini matokeo yake wachezaji wanashindwa kuwanyanyu wapenzi na mashabiki wao kewnye viti. Lost-9fm iliamua kufunga safari hadi kwenye moja ya viwanja mjini kahama na kufanya mahojiano na mmoja kati ya vijana waliohodhulia mazoezi uwanjani hapo. Mmoja kati ya vijana hao alisema kuwa vijana wanapewa nafasi ktk mpira wa miguu lakini wanashindwa kuonyesha vipaji vyao kwahiyo tunaiomba serikali ituangalie na sisi vijana tunaopenda na ambao tuna vipaji vya mpira wa kikapu, ni maneno yake kijana aliyejitambulisha kwa jina la Kubwaje ama kubwa kalimenze kama anavyofahamika kwa wakazi wa mjini kahama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment