Kitendo cha msanii wa filamu Rose Ndauka kila wakati kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na waume za wa watu, kimedaiwa kummaliza huku mwenyewe akitafuta njia sahihi ya kukabiliana na hali hiyo bila mafanikio.
Rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa maelezo kuwa yeye siyo msemaji wake alilitonya Amani kuwa, Rose amekuwa akiumizwa na hali hiyo huku mwenyewe akidai kuwa, hapendi lakini anashangaa waume za watu ndiyo wanaoyashikilia maisha yake ya kimapenzi.
“Mnaweza kudhani anafanya makusudi kuchukua waume za watu lakini huwezi kuamini mwenyewe hafurahishwi na tabia hiyo, yaani anajikuta tayari yuko kwenye penzi na mume wa mtu na ni jambo linaloutesa moyo wake sana.
“Anahisi hautendei haki moyo wake kwa ‘kudokoa’ vya watu lakini mwisho wa siku anakuwa hana jinsi, anabaki kuumia tu, mkiongea naye anaweza kuwaeleza kinagaubaga,”alisema mtoa habari huyo.
Baada ya habari hiyo kutua mezani kwetu, Mwandishi wetu alimtafuta Rose kupitia simu yake ya kiganjani, alipopatikana alikuwa na haya ya kusema;
Nashindwa pa kuanzia katika kulizungumzia hili ila jambo hili linautesa sana moyo wangu, ukiangalia historia yangu waume za watu ndiyo ambao wanaoyashika maisha yangu na ndiyo ninaodumu nao.
Huwa natamani kuwa na mwanaume wa kwangu lakini kila nikijaribu nashindwa,” alisema Rose na kufafanua:
“Mwanzo kabisa nilikuwa na uhusiano na mume wa mtu, akanisumbua nikaachana naye, baadaye tena nikajikuta nimeangukia kwa mwingine ambaye naye ni mume wa mtu, huyu alikuwa na visa vingi lakini nilikuwa nampenda.
“Naye ikafika wakati tu
kaachana, nikahamia kwa mwingine ambaye hakuwa mume wa mtu lakini nilimfumania mara tatu. Naye nikaachana naye na sasa huwezi kuamini mwanaume anayetaka kunioa ni mume wa mtu, sijui kuna siri gani katika hili lakini natamani kuwa na wa kwangu pekee,”alieleza msanii huyo.
No comments:
Post a Comment