
Kwa taarifa nilizonazo Rais Kagame ameweza kuibadili Rwanda kwa kiwango kizuri sana ikiwa ni pamoja na nchi kuwa safi, kukua kiuchumi, kujengeka kimpangilio pamoja na ishu nyingine, sasa hivi sehemu kubwa ya mji wa Kigali umejengwa kwa mujibu wa ramani inayotakiwa, nyumba za kuishi zilizo kwenye mpango kama miji mingine ya nchi zilizoendelea, pamoja na barabara za ndani za Kigali kuwekwa mawe kitaalamu kuondoa vumbi kwenye mji.



Hii ndio Account ya Rais Paul Kagame kwenye twitter, Paul Kagame (54) ni rais wa sita wa nchi hiyo ambayo ameiongoza kwa zaidi ya miaka kumi na wengi wanaamini kama angeendelea kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi, angeweza kuibadilisha Rwanda kwa kiwango kikubwa sana
No comments:
Post a Comment